Psalms 67

Mataifa Yahimizwa Kumsifu Mungu

(Kwa Mwimbishaji: Na Ala Za Nyuzi Za Muziki. Zaburi. Wimbo)


1 aMungu aturehemu na kutubariki,
na kutuangazia nuru za uso wake,

2 bili njia zako zijulikane duniani,
wokovu wako katikati ya mataifa yote.


3 cEe Mungu, mataifa na wakusifu,
mataifa yote na wakusifu.

4 dMataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe,
kwa kuwa unatawala watu kwa haki
na kuongoza mataifa ya dunia.

5 eEe Mungu, mataifa na wakusifu,
mataifa yote na wakusifu.


6 fNdipo nchi itatoa mazao yake,
naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.

7 gMungu atatubariki
na miisho yote ya dunia itamcha yeye.
Copyright information for SwhKC